Showing posts with label Mgomo wa Madaktari. Show all posts
Showing posts with label Mgomo wa Madaktari. Show all posts

Saturday, 30 June 2012

Huu ndiyo uamuzi wa Serikali juu ya mgomo....Tunajenga au Tunabomoa?


Serikali yaomba madaktari nje ya nchi
•  Bilioni 200 zatengwa kuwalipa

na Martin Malera, Dodoma
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.
Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia  madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama  Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.
Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.
Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.
Hata hivyo, uamuzi wa serikali  kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.
Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda  kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.
Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda  alisema serikali  haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani.
“Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?” alihoji Dk. Kigwang’ala.
Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza  kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.
Jeshi lachukua nafasi za madaktari
Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.
Juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.
Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Kikosi ya 521, Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila vikwazo.
“Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu labda kwa asilimia 90.
Mgawe alisema madaktari wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake, hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.

Polisi Tanzania itakamata madaktari wanaogoma

JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA LIMESEMA IJUMAA KUWA LITAANZA KUWAKAMATA MADAKTARI WANAOSHIRIKI KATIKA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI HUMO KWA SABABU WANAKIUKA AMRI YA MAHAKAMA.


SERIKALI YA TANZANIA KUPITIA KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ILIWEKA PINGAMIZI SIKU MOJA KABLA YA MADAKTARI HAO KUANZA MGOMO JUNI 23 KUZUIA MGOMO HUO. LAKINI HATA HIVYO MGOMO HUO UMEKUWA UKIENDELEA KWA ZAIDI YA WIKI MOJA SASA.

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI IJUMAA JIJINI DAR ES SALAAM, KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO PAUL CHAGONJA ALISEMA JESHI LA POLISI LINA KILA SABABU YA KUWAKAMATA MADAKTARI WANAOGOMA. ALISEMA KAMA MADAKTARI HAWAKUKUBALIANA NA PINGAMIZI YA SERIKALI WALIKUWA NA HAKI YA KUKATA RUFAA SIO KUENDELEA NA MGOMO.

KATIKA HABARI NYINGINE MADAKTARI WANASEMA DR. STEVEN ULIMBOKA AMBAYE ALITEKWA NA KUPIGWA NA WATU WASIOJULIKANA MAPEMA WIKI HII ANAHITAJI KUFANYIWA VIPIMO ZAIDI NJE YA NCHI.

WAKATI HUO HUO, MADAKTARI BINGWA WA SERIKALI ZA UMMA IJUMAA WALITANGAZA KUJIUNGA NA MGOMO KUPINGA KUPIGWA KWA DR. ULIMBOKA. JESHI LA POLISI LIMEUNDA TUME WATU WATANO KUFANYA UCHUNGUZI WA MKASA WA DR.

 ULIMBOKA LAKINI TUME HIYO IMEPINGWA NA WENGI IKIWA NI PAMOJA NA MADAKTARI WENYEWE.

Chanzo - Voice of America

HIKI NDICHO WANACHOKISEMA MADAKTARI BINGWA, SASA NI HATARI!!

TAMKO LA MADAKTARI MABINGWA WA MKOA WA DAR ES SALAAM
(MNH, MOI, OCEAN ROAD NA HOSPITALI ZA MANISPAA YA MKOA WA DAR ES SALAAM)


Kutokana na kikao kilichofanyika leo tarehe 29/06/2012, Madaktari mabingwa tumeamua yafutayo:

Tunalaani kwa kauli moja kitendo alichofanyiwa Daktari na Kiongozi wa Jumuiya yetu, Dkt. Steven Ulimboka, cha kutekwa, kuumizwa na kutupwa msitu wa Mabwepande. Kitendo hiki kimetuhuzunisha, kimetufadhaisha na kutufanya kuishia katika hofu ya hali ya juu.
Tunazitaka Mamlaka husika kutuhakikishia mustakabali wa usalama wetu sasa na siku za mbeleni katika nchi yetu.
Tunalaani juhudi zinazofanywa na wadhalimu wote katika fani ya Udaktari.
Tunalaani vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa Madaktari wenzetu sehemu mbalimbali kama Bugando, Dodoma na Mbeya pamoja na kwingineko.
Tunatamka wazi kuwa kitendo cha kuwafukuza, kuwanyima mishahara na haki nyingine za mwezi Juni, ni udhalilishaji na kinyume na amri ya mahakama.
Kutokana na vitendo vyote tajwa hapo juu, (yaani kutekwa na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka, Unyanyasaji wa Madaktari wenzetu) na pia kutokana na ukweli kwamba hali ya Dkt. Ulimboka inazidi kudorora; vile vile kwa kuwa siku zote Serikali imekuwa ikikubali kuwa madai yetu ni ya msingi (lakini haiyatafutii ufumbuzi wowote), TUMEAMUA KUSIKISHA KUTOA HUDUMA KATIKA HOSPITALI ZOTE TUKAZOFNYIA KAZI, yaani Muhimbili, MOI, Ocean Road, Amana, Mwananyamala, n.k. hadi hapo madai yetu ya msingi yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
Tunaomba Madaktari mabingwa wote hapa nchini watuunge mkono katika harakati hizi za kuboresha sekta nzima ya afya.

IMETOLEWA NA
DKT. C. MNG’ONG’O
MWENYEKITI WA MADAKTARI MABINGWA - KANDA YA DAR ES SALAAM

Source:wavuti.com

Friday, 29 June 2012

MADAKTARI 72 WA HOSPITALI YA RUFAA WALIOGOMA WATIMULIWA KAZI -MBEYA


 Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari,wakifuatilia taarifa kamili za madaktari waliofukuzwa kazi Mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr  E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya(Picha na Mbeya Yetu)
*******
Habari na Godfrey Kahango,Mbeya.
Sakata la mgomo wa Madaktari  katika hospitali ya Rufaa Mbeya, limeendelea kuingia katika sura mpya baada ya Madaktari 72, waliogoma kutimuliwa na bodi ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya.

Hatua ya kutimuliwa  kwa madaktari hao imekuja baada ya bodi hiyo kuwaandikia barua ya kuwataka  kukaa meza moja na kujadili mstakabali mzima wa madai yao ambapo wadaktari hao kukaidi wito huo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dr. Norman Sigalla, alisema kuwa wameamua kusitisha Mkataba wa madaktari hao na kuwarudisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

”Madaktari 54  ni wale walioko kwenye mafunzo ya vitendo kwa mkataba wa miaka miwili  na hospitali ya Rufaa  na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya” alisema Sigalla na kuwataka wale wote wanaoishi bwenini hospitalini hapo kuwa ifakapo saa 11:00 jioni ya leo(jana) wawe wameondoka katika eneo hilo la hospitali”alisema.

Alisema kuwa wamefikia hatua hiyo kwa kuwa madaktari hao wamekiuka , kuvunja mkataba wawalioingia  na hospitali hiyo pia kukiuka kanuni za kudumu za Umma na toleo la 2009, kifungu namba F16- F. 17 na F27.

 Alisema kuwa madaktari hao waliandikiwa barua ya mara ya kwanza ya kuwaita ili wakutane na Mwenyekiti wa bodi hiyo ya rufaa mbeya lakini walikaidi na kuandikiwa barua ya pili ya kuwataka waeleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kutofika kazini kwa siku tano lakini nayo waliikaidi.

Dr. Sigalla akizungumzia kuhusu madaktari  18 ambao ni waajiriwa pia wamo katika mgomo huo alisema kuwa nao wanakabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira zao hospitalini hapo na kuwarudisha Wizarani kwa katibu Mkuu  Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa hatua  stahiki za kinidhamu.

“Madaktari waajiriwa wanakabidhiwa barua zao za kusimamishwa ajira yao hospitalini hapa na kuwarudisha Wizarani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi  wa Jamii kwa hatua stahiki za kinidhamu” alisema Dr. Sigalla.

Hata hivyo gazeti hili lilishuhudia baadhi ya  madaktari hao wakiondoka kwenye mabweni yao huku madaktari hao wakisikika wakisema wapo tayari kurudi walikotoka na kwamba hawapo kuvumilia kile kinachoendelea hivi sasa.

“Tupo tayari kuondoka hospitalini hapa na kurudi tuliko toka wala hatutishiki hata kidogo” walisikika wakisema huku wakiwa wanapakia mabegi yao kwenye tax walizokodi. 

Wakati huohuo Jeshi la Polisi mkoania hapa lilizingira eneo la Hospitali ya Rufaa kuimarisha ulinzi na usalama. 
Source: CHIMBUKO LETU BLOG