JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA LIMESEMA IJUMAA KUWA LITAANZA KUWAKAMATA MADAKTARI WANAOSHIRIKI KATIKA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI HUMO KWA SABABU WANAKIUKA AMRI YA MAHAKAMA.
SERIKALI YA TANZANIA KUPITIA KWA
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ILIWEKA PINGAMIZI SIKU MOJA KABLA YA
MADAKTARI HAO KUANZA MGOMO JUNI 23 KUZUIA MGOMO HUO. LAKINI HATA HIVYO
MGOMO HUO UMEKUWA UKIENDELEA KWA ZAIDI YA WIKI MOJA SASA.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA
HABARI IJUMAA JIJINI DAR ES SALAAM, KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO
PAUL CHAGONJA ALISEMA JESHI LA POLISI LINA KILA SABABU YA KUWAKAMATA
MADAKTARI WANAOGOMA. ALISEMA KAMA MADAKTARI HAWAKUKUBALIANA NA PINGAMIZI
YA SERIKALI WALIKUWA NA HAKI YA KUKATA RUFAA SIO KUENDELEA NA MGOMO.
KATIKA HABARI NYINGINE MADAKTARI
WANASEMA DR. STEVEN ULIMBOKA AMBAYE ALITEKWA NA KUPIGWA NA WATU
WASIOJULIKANA MAPEMA WIKI HII ANAHITAJI KUFANYIWA VIPIMO ZAIDI NJE YA
NCHI.
WAKATI HUO HUO, MADAKTARI BINGWA
WA SERIKALI ZA UMMA IJUMAA WALITANGAZA KUJIUNGA NA MGOMO KUPINGA
KUPIGWA KWA DR. ULIMBOKA. JESHI LA POLISI LIMEUNDA TUME WATU WATANO
KUFANYA UCHUNGUZI WA MKASA WA DR.
ULIMBOKA LAKINI TUME HIYO IMEPINGWA NA WENGI IKIWA NI PAMOJA NA MADAKTARI WENYEWE.
Chanzo - Voice of America
No comments:
Post a Comment