HIKI NDICHO WANACHOKISEMA MADAKTARI BINGWA, SASA NI HATARI!!
TAMKO LA MADAKTARI MABINGWA WA MKOA WA DAR ES SALAAM
(MNH, MOI, OCEAN ROAD NA HOSPITALI ZA MANISPAA YA MKOA WA DAR ES SALAAM)
Kutokana na kikao kilichofanyika leo tarehe 29/06/2012, Madaktari mabingwa tumeamua yafutayo:
Tunalaani kwa kauli moja kitendo alichofanyiwa Daktari na Kiongozi wa
Jumuiya yetu, Dkt. Steven Ulimboka, cha kutekwa, kuumizwa na kutupwa
msitu wa Mabwepande. Kitendo hiki kimetuhuzunisha, kimetufadhaisha na
kutufanya kuishia katika hofu ya hali ya juu.
Tunazitaka Mamlaka husika kutuhakikishia mustakabali wa usalama wetu sasa na siku za mbeleni katika nchi yetu.
Tunalaani juhudi zinazofanywa na wadhalimu wote katika fani ya Udaktari.
Tunalaani vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa Madaktari wenzetu
sehemu mbalimbali kama Bugando, Dodoma na Mbeya pamoja na kwingineko.
Tunatamka wazi kuwa kitendo cha kuwafukuza, kuwanyima mishahara na haki
nyingine za mwezi Juni, ni udhalilishaji na kinyume na amri ya
mahakama.
Kutokana na vitendo vyote tajwa hapo juu, (yaani kutekwa
na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka, Unyanyasaji wa Madaktari wenzetu) na pia
kutokana na ukweli kwamba hali ya Dkt. Ulimboka inazidi kudorora; vile
vile kwa kuwa siku zote Serikali imekuwa ikikubali kuwa madai yetu ni ya
msingi (lakini haiyatafutii ufumbuzi wowote), TUMEAMUA KUSIKISHA KUTOA
HUDUMA KATIKA HOSPITALI ZOTE TUKAZOFNYIA KAZI, yaani Muhimbili, MOI,
Ocean Road, Amana, Mwananyamala, n.k. hadi hapo madai yetu ya msingi
yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
Tunaomba Madaktari mabingwa wote hapa nchini watuunge mkono katika harakati hizi za kuboresha sekta nzima ya afya.
IMETOLEWA NA
DKT. C. MNG’ONG’O
MWENYEKITI WA MADAKTARI MABINGWA - KANDA YA DAR ES SALAAM
Source:wavuti.com
No comments:
Post a Comment