|
Tumaini Msowoya, Iringa WIMBI la viongozi na makada wa CCM kuhamia vyama vya upinzani linaendelea kukitikisa chama hicho, baada ya viongozi wa chama hicho mikoa ya Iringa na Singida kujiunga Chadema.Chadema kimewateka makada hao kilipofanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Kihesa Sokoni, juzi mjini Iringa kwa lengo la kuendeleza mkakati wake wa Movement For Change-M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) na kufafanua bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13.Wimbi la makada wa CCM kuhamia Chadema lilipamba moto Aprili mwaka huu baada ya Ole Millya kuondoka akifutiwa na viongozi kadhaa wa chama hicho, akiwamo Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Longido, wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wa CCM wilayani Ngorongoro. Viongozi wa CCM waliojiunga Chadema jana, ni Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Iringa Vijijini, Yohana Mwena na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani humo. Wengine ni Katibu wa UV-CCM Mkoa wa Singida anayesoma katika Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco) kilichopo Iringa, Kasifia Sumpta, mwanazuoni wa chuo hicho, Dk Matabazi Lugazia, na kada wa siku nyingi wa chama hicho, Zuberi Mwachura ambaye alirejesha kadi sita za CCM kutoka katika familia yake. Licha ya Chadema kupewa kibali cha kufanyia mkutano huo kwenye uwanja mdogo uliozungukwa na barabara zenye magari mengi, umati wa watu ulifurika, huku wengine wakilazimika kukaa juu ya nyumba na miti. Katika mkutano huo ambao ulihutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James ole Millya na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, wanachama wengine zaidi ya 200 wa CCM walirudisha kadi na kujiunga na Chadema. Mbali na shughuli ya kupokea wanachama hao kwa mtindo wa ‘kuvua gamba na kuvaa gwanda’, viongozi wa Chadema waliichambua bajeti ya Serikali inayoanza kujadiliwa bungeni leo, wakifafanua ni kwa jinsi gani haitamnufaisha mwananchi wa kawaida. Waliovua gamba Wakizungumza wakati wakirudisha kadi hizo, makada na viongozi hao walisema kuwa, wameamua kufanya hivyo baada ya kuchoshwa na sera za CCM, ambazo walidai kuwa hazitekelezeki. Akizungumzia kuhama kwake CCM, Mwena alisema amechoka kuona rasilimali za taifa haziwanufaishi wananchi, badala yake zinawanufaisha matajiri, huku kukiwa na tofauti kubwa ya kipato. “Mwenzenu nimevumilia nimeshindwa, leo nimeamua kuondoka CCM, nimechoka kuona sera ambazo hazitekelezeki, huku wananchi maskini wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa wakati kuna rasilimali nyingi za taifa zinazoliwa na matajiri,” alisema Mwena. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi Mji wa Iringa na vitongoji vyake, baadhi ya waliopewa nafasi kueleza kero zao walisema, hawaikubali bajeti iliyosomwa hivi karibuni kwa kuwa haijalenga kuwasaidia wananchi maskini. “Bajeti iliyosomwa inataja kupandisha kodi ya pombe na sigara, ikimaanisha kuwa uchumi wetu unategemea vilevi hivyo, hivi Watanzania tukigoma kunywa pombe ina maana Serikali itashindwa kujiendesha, bajeti iliyosomwa tunaikataa na tunawaagiza mkawaeleze, kuwa hiyo imelenga kuwaneemesha wao na siyo sisi maskini,” alisema Yohana Mkule, mkazi wa manispaa hiyo. Kutokana na wananchi wengi, kuigomea bajeti hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliwaunga mkono, huku akiahidi kuwa Kambi ya Upinzani haitakubali bajeti hiyo ipitishwe. “Uwendawazimu ni kufanya jambo lilelile, kwa njia zilezile huku ukitegemea matokeo tofauti. Serikali inatumia njia zilezile ikidhani mfumko wa bei unaweza kupungua, huu ni uwendawazimu, nawatoa hofu kwa sababu hatutakubali bajeti hii ipitishwe,” alisema Kabwe. Alisema vitu vinavyofanya maisha ya Watanzania kuwa magumu ni mfumko wa bei, hasa katika vyakula ambao ni asilimia 25, na nishati ambayo ni asilimia 27, huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo kwa kuandaa bajeti inayolenga kukomoa wananchi. Hata hivyo, aliwataka wakazi wa Iringa kuendelea kuwa wavumilivu wakati mbunge wao atakapokuwa akifanya kazi za kuleta mabadiliko katika maeneo mengine, ili kukiandaa chama hicho kushika dola mwaka 2015. Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya aliwataka wakazi wa Manispaa ya Iringa kutoendelea kuivumilia CCM ambayo imeshindwa kutambua kitu gani wananchi wake wanataka. “Mimi niliondoka baada ya kuona hoja zangu hazifanyiwi kazi ndani ya CCM, nimeingia Chadema nikitarajia mabadiliko makubwa kwa nchi yangu, msikubali kuumia, lazima tulete mabadiliko,” alisema. Millya alisema nchi nyingi ikiwamo Kenya zimeving’oa vyama tawala, isipokuwa Tanzania ambayo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 lengo hilo litatimia. Mbunge wa Iringa Mjini, Msigwa alisema viongozi wa Chadema wameamua kugawana siku za mwisho wa wiki kufanya kazi za chama hicho kutokana na mkutano wa Bunge unaoendelea katika siku za kawaida. |
Showing posts with label Chadema. Show all posts
Showing posts with label Chadema. Show all posts
Monday, 18 June 2012
Chadema yavuna vigogo wa CCM::Mwananchi
Chadema prepares for 2015 elections
The opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) has started preparations for the 2015 general elections, its national chairman Freeman Mbowe has said.
Chadema National Chairman Freeman Mbowe
“Whoever wants to run for any position should now send an application, curriculum vitae and passport size photograph to the party headquarters for screening,” Mr Mbowe told a news conference in Dodoma on Sunday.
He said Chadema would not wait for those who fail to secure nomination during preliminary polls for councillorship or parliamentary seats in other political parties as was the case in the past. Recruiting people who have failed in other parties leads to indiscipline and conflicts within the party.
“We want clean and diligent people who are ready to work as a team and respect the party’s constitution,” he stressed.
However, observers view the move as having been influenced by Mr John Shibuda’s antics, especially after being quoted as saying that he had plans of running for president come 2015.
Meanwhile, Mr Mbowe alleged students in universities and other institutions of higher learning who are members of Chadema were being harassed or expelled. He said that he would call upon the government to protect such students to ensure that they complete their studies.
“We are going to move a motion asking the government to present a statement on protection of such students in the National Assembly,” he said during a meeting with students who are Chadema members. Mr Mbowe also used the opportunity to wish well students who begin their final examinations on Monday.
He asked the students to return to their home villages and open Chadema branches. “We want to have a party branch in every ward and village in the country. Our strategy is to reach the masses at the grassroots,” Mr Mbowe told the students.
He urged the students not to fear anybody in the political struggle. “Our goal is to form the government soon and lead this country,” he said, adding that: “Personally I have five cases pending in court.” He said every month he has to appear before courts two or three times.
Reading the students’ message, Ms Pasquiha Ferdinand, a second year Barchelor of Education student at St. John University, said Chadema members risked expulsion. She said expulsions started at the University of Dodoma (UDOM) and St. John appears to be the next in line. Ms Ferdinand also asked Chadema to assist students with cases in meeting legal costs.
Source Tanzania Daily News
Subscribe to:
Posts (Atom)