ZIKIWA zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Njombe kusini Anne Makinda ambaye ni spika wa bunge kutangaza kutogombea ubunge tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015,mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com waibuka na siri nzito za mbunge huyo kuiogopa nafasi hiyo tena.
Baadhi ya wana CCM na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) wameanika siri hiyo ya Makinda kutangazwa kuto gombea kuwa ni kutokana na kuogopa kuja kung'olewa kwa aibu katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake mdogo wa kuwatumikia wapiga kura wake .
Huku wana chama wa CCM wa jimbo la Njombe kusini wakidai kuwa Makinda walianza kumchoka kutokana na kushindwa kufanya mambo ya kimaendeleo katika jimbo hilo na hivyo kusababisha jimbo hilo kuwa ngome ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Kwani wamedai kuwa pamoja na jimbo hilo kuongozwa na mbunge Makinda ambaye pia ni spika wa bunge ila kasi ya maendeleo katika jimbo hilo haipo na kama jimbo halina mbunge kutokana na mbunge wao huyo kuonekana kuegemea mambo ya kitaifa zaidi huku jimboni kwake mambo yanakwenda kombo .
"Hatukutegemea jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Deo Filikunjombe ni kijana mchanga katika siasa kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo kwa kipindi kifupi toka alipoingia madarakani uchaguzi wa mwaka 2010 .....huku mbunge wetu spika Makinda akishindwa hata kutengeneza barabara za jimboni kwake na kuwa barabara mbovu kuliko hata za wilaya ya Ludewa na zile za wilaya ya Makete" alisema John Sanga mkazi wa Njombe mjini
Alisema kuwa zamani jimbo la hilo la Njombe kusini bendera za vyama vya upinzani zilikuwa za kutafuta ila ukipita leo katika jimbo hilo la Makinda utitiri wa benderea za Chadema vijijini na mjini unaweza kufikiri ni ngome ya Chadema.
Sanga alisema kuwa hatua ya mbunge wao huyo kuwa mbunge wa kwanza wa CCM kutangaza kutogombea ni baada ya kuona hali ya upepo wa kisiasa kwake kuwa mbaya zaidi na hata akiwa katika ziara zake jimboni wananchi wamekuwa hawamkubali kivile.
Hata hivyo alisema jimbo la Njombe kusini ambalo mbunge wake Makinda limeendelea kuwa nyuma kimaendeleo na kupitwa na jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Fikunjombe ameendelea kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo ukilinganisha na mbunge wao Makinda ambaye amekuwa ni mtalii katika jimbo hilo .
"Tunamshangaa sana mbunge wetu Makinda kwa uamuzi wake wa kutangaza kutogombea .... kiukweli hata asingetangaza msimamo wetu wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini japo hatukuweka wazi ila ilikuwa ni kumpiga chini katika kura za maoni sisi kwa sasa mbunge wetu ni kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe Deo Mwanyika ambaye amekuwa akiendelea kuhamasisha maendeleo jimboni "
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchugaji Msigwa alisema kuwa Makinda ni sawa na mfa maji ambaye kimsingi haishi kutapa tapa kwani kauli yake ya kuwa wabunge nusu walitaka kujiuzulu kwa sakata la posho ni uongo mtupu na kuwa yeye ametumia kisingizio cha posho kuweza kueleza nia yake ya kutogombea ubunge ila ukweli Makinda amebanwa sana na Chadema katika jimbo lake.
Mbunge Msigwa alisema moja kati ya mikakati ya Chadema ni kuhakikisha inachukua majimbo mengi zaidi katika mkoa wa Iringa na moja kati ya majimbo ambayo ni rahisi zaidi kwa Chadema kushinda ni pamoja na jimbo hilo la Makinda ambalo wapiga kura wa jimbo hilo hawataki kabisa kusikia Makinda wala CCM.
"Makinda asijitetee kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kupisha wanachama wengine kuongoza ama kwa ajili ya posho ya wabunge ....anapaswa kusema wazi kuwa jimbo hilo limemshinda kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wapiga kura wake"