Elizabeth Michael (Lulu) |
Leo hakutakiwa kujibu
lolote, kesi imeahirishwa hadi Aprili 24 mwaka huu, amerudishwa rumade
kutokana na kesi za mauaji hazina dhamana. Ungana nasi baadaye kwa
habari zaidi.
Alichoeleza Lulu polisi hiki hapa
MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa
kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa
nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.
Habari zilizopatikana jana
kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa
kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu
kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.
"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa
baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake
hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia
simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.
"Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.
Chanzo kiliongeza kuwa tangu
Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote
hata katika mahojiano na polisi.
Katika hatua nyingine, Polisi wa
kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana
waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai
wanamtaka Lulu.
"Tunataka
jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya
Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo
kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa
kutuliza ghasia kama zingezuka.
Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa,
Msanii
Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa
mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili
jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni
mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa
Serikali.
“Tunasubiri ripoti ya Mkemia
Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya
sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana).
Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema
Kenyela.
Aliongeza ripoti hiyo itaweza
kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.
Kamanda Kenyela alisema kuwa,
ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba
amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.
Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu.
No comments:
Post a Comment