Sunday, 18 March 2012

BBC: Mtengeza filamu ya Kony zamruka


Jason Russel

Mkurugenzi wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.

Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.
Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana Russell.
Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.
Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.

No comments:

Post a Comment