Usaili huo ni kwa niaba ya Mamlaka za Ajira zifuatazo;- Dar es Salaam Maritime Institute (DMI), Tanzania Institute of Education (TIE), Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), Kibaha Education Centre (KEC), Eastern Africa Statistical Training Centre (EASTC), Tanzania Commission for Universities (TCU) na Occupational Safety and Health Authority (OSHA), Tanzania Government Flight Agency (TGFA), Government Chemist Laboratory Agency (GCLA), Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology (CAMARTEC) na Ardhi University (ARU).
Daudi amesisitiza waombaji wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika tangazo hususani kuhusu sehemu ya kufanyia usaili, muda wa kuwasili katika sehemu ya usaili, kubeba vyeti na viambatisho vyote muhimu vinavyohitajika katika usaili. Aliongeza kuwa kwa matangazo ya baadhi ya nafasi za kazi za Wizara na Taasisi nyingine zilizokuwa zimetangazwa katika tarehe hizo maombi yake yako katika hatua za mwisho za mchakato na waombaji waliokidhi vigezo watatangaziwa hivi karibuni tarehe za kuitwa kwenye usaili.
Aidha, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwatangazia fursa nyingine za ajira katika Utumishi wa Umma wadau wote wenye kutafuta kazi kuangalia Matangazo mawili tofauti la Kiingereza na Kiswahili yaliyoko upande wa kushoto wa tovuti ya Sekretarieti ya Ajira.
Mwisho amesema kuwa ni muhimu waombaji wa fursa za ajira wajue kuwa changamoto ya ajira ni kubwa hivyo ni vyema wale wanaopata fursa za kusoma wakazitumia vizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani katika soko la ajira pindi wanapoitwa kwenye usaili hali itakayowasaidia kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata ajira.
16/11/2012; Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Bofya PDF hapa chini kuona nafasi zilizotangazwa pamoja na majina ya wanaoitwa kwenye usaili
No comments:
Post a Comment