RPC wa Kinondoni- ACP Charles Kenyela akiongea na waandishi wa habari.
POMBE kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha
kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba
aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba
uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na
uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi. ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba
wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba.
Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana
akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao
wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.
Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema
kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati
akizungumza na simu. “Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa
sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku
akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje
ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na
kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani
na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa
maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema
Kamanda huyo.
Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba
kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta
wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.
Source:
No comments:
Post a Comment