KANUSHO LA HABARI POTOFU KATIKA TANZANIA DAIMA AMBALO LEO LINA KICHWA CHA HABARI KISOMEKACHO "JK.ALINDA MAWAZIRI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti
la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika
ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’,
inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi
ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Habari hiyo imedai kuwa Mhe.
Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta
uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “Rais
Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa
suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita”
Tunachukua nafasi
hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo gazeti la Tanzania Daima
Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
Mheshimiwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi
nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonanawala
kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma
Mhe Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.
Pia
ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika
kutekeleza kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo
wanavyofanyia kazi pamoja na taaluma yenyewe.
Mwisho
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Aprili, 2012