Februari tarehe kumi na nne ni siku ya wapendanao au Valentine, lakini
siku hii ikiadhimishwa kote duniani kwa raha, baadhi ya waume nchini
kenya hawaifurahi kwani wanapigwa na kunyanyaswa na wake zao.
Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini humo
Nderitu Njogu, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.
Bw Nderitu anasema utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za
kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasabibisha kuwadharau
wanaume.
Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya
kuwa wanawake wengi sasa wana kipato kikubwa kuliko waume zao.
Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri
huko mkoa wa kati, baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa
panga.
Mwanamume huyo bado anapokea matibabu hospitalini baada ya kukatwa katwa usoni. uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.
Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake
zao mwaka jana. Anasema utafiti wa shirika lake unaonyesha kesi nyingi
za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika mkoa wa kati.
"Siku hii ya Valentine na washauri wanaume
wasikubali kudhalalishwa na wake zao, kwa kufanya matumizi makubwa
kuliko na wanayoweza kumudu" alisema Bw Nderitu.
~BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment