Monday, 13 February 2012

IRINGA, MZIMU WA MKWAWA UNAFANYA KAZI?

Upo usemi miongoni mwa wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa kifo alichokufa babu yao Mkwawa kilikuwa ni cha kishujaa! Kujiua ni ujasiri?


Hivi ndivyo mzimu huo  umeendelea kufanya kazi baada ya kijana Raphael Steven (20) mkazi wa Mwangata Iringa kujinyonga kwa kutumia khanga ya mama yake chumbani kwa mamaye. Kijana Raphael Steven aliyekuwa akisajili laini za tigo imenenwa kuwa enzi za uhai wake hakuwa na makuu na mtu na ni kijana aliyependwa na majirani. Wakiongea na kituo cha redio cha Ebony FM mama wa marehemu na bibi wa marehemu wadai kusikitishwa na kifo hicho na kueleza kuwa hawajaelewa hasa nini chanzo cha kijana wao kujiua.


(tunaomba radhi kwa picha hizi)
Kijana Raphael akiwa katika sura ya ""ujasiri"  inasikitisha sana

 Baadhi ya mashuhuda na waandishi wa habari wakichukua picha za marehemu
 Ujumbe ulioachwa na marehemu
Raphael (kushoto) enzi za uhai wake.
(picha zote na Francis Godwin)


Kwa mujibu  wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa kijana huyo mchana wa jana alionekana mtaani akiwa na mawazo tele na hakuwaa na muda wa kuzungumza na mtu kama siku za mwanzo .

Hata hivyo mashuhuda hao walisema kuwa kwa siku ya jana kijana huyo alionekana katika ukumbi mmoja wa starehe na kuzuiwa kuingia katika ukumbi huo baada ya kukosa kadi ya mwaliko .


Zipo habari zinazodai kuwa kijana huyo amekufa kifo kama kile cha baba yake mzazi aliyekufa kwa kujinyonga mwaka 2002 kwa wakati huo walikuwa wakiishi eneo la Isoka mjini Iringa.Mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kukuta ujumbe wa maandishi ambao marehemu huyo alipata kuuacha kabla ya kifo chake katika meza ya chumba chake na katika ujumbe huo amepata kuacha maneno mazito yakiwemo ya kutaka asisumbuliwe mtu yeyote kwa kifo chake na kuwa kuwaaga baadhi ya marafiki na mpenzi wake mmoja pamoja na mama yake mzazi na kudai kuwa maisha ya Dunia Jembe lenu natangulia nilikotokea."Asisumbuliwe mtu kwa kifo changu na na kutaja majina ya rafiki zake na mpenzi wake (ambayo yamehifadhiwa huku akimalizika na neno .Respect..Don't Cry Momy and Rukia!!...Pole mama nimeamua kumfuata baba angu!!" ulisomeka ujumbe huo ambao ameacha marehemu

No comments:

Post a Comment