Monday, 5 March 2012

MSHUHUDIE LINNAH AKIWA ZIARANI U.S.A

Chanzo: Swahilivilla Blog

  
Kwa wale wasiomjua mwanamuziki wa kizazi kipya anaejulikana kwa jina la  "Linah  ndilo jina lake analotumia katika kazi zake za sanaa.

Yupo ndani ya Jiji amewasili siku chache tu zilizopita, Msanii Linah atakuwa nchini Marekani mpaka mwezi wa May 30, katika ziara yake ya muziki na amejianda rasmi kutumbuiza, Washington DC na kama majimbo 9 ya mengine ya Nchini Marekani.

Vile vile Linah alibahatika kukutana na mwana harakati wa blog ya changamotoyetu, Anko Mubelwa Bandio kwa mahojiano mafupi na msanii huyo, alipozungumzia kuhusu historia yake kimuziki na maendeleo katika muziki wa kizazi kipya pamoja na ziara yake rasmi kwa burudani.

Mahojiano hayo yalifanyika siku jumamosi March 3, 2012 ndani ya Hampton Inn College Park Jijini Maryland  hapa Marekani.