Friday 2 November 2012

KUITWA KWENYE USAILI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
31 Oktoba, 2012
Kumb. Na. EA.7/96/01/C/61
KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ocean Road Cancer
Institute (ORCI) na Muhimbili Othopaedric Institute (MOI) anatarajia kuendesha usaili na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatangazia waombaji wa fursa
za ajira kwa tangazo lililotolewa tarehe 28/05/2012 za Ocean Road Cancer Institute (ORCI)
na Muhimbili Othopaedric Institute (MOI kuwa wamechaguliwa kufanya usaili.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1. UKAGUZI WA VYETI UTAANZA SAA 1:00 HADI 1:30 ASUBUHI SIKU YA MTIHANI
WA MCHUJO.
2. KUJA NA KITAMBULISHO KWA AJILI YA UTAMBUZI MFANO: KITAMBULISHO
CHA MKAZI, KUPIGIA KURA, BENKI, KAZI, HATI YA KUSAFIRIA N.K
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) za kuanzia kidato cha nne, sita,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
mwombaji.
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
5. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi
zitakapotangazwa.
source www.ajira.go.tz

No comments:

Post a Comment