Sunday, 11 March 2012

Mmarekani auwa raia 15 wa Afghanistan

Mwanajeshi wa Marekani aliyehemkwa, aliuwa raia 15 majumbani mwao, wakiwemo watoto tisa, katika jimbo la Kandahar, Afghanistan, Jumapili alfajiri.
Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan


Mwanajeshi huyo anazuwiliwa na inasemekana alipagawa kabla ya mauaji hayo.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta, alisema amesikitishwa sana na tukio hilo.
Mauaji hayo yametokea wakati kuna mvutano katika uhusiano baina ya Waafghani na wanajeshi wa Marekani, baada ya Kurani kuchomwa kwenye kambi ya Marekani mwezi uliopita, na kuzusha maandamano ya ghasia sehemu mbali mbali za nchi.
BBC-SWAHILI

No comments:

Post a Comment