Tuesday, 20 March 2012

BREAKING NEWS; DIWANI WILAYA YA LUDEWA AJINYONGA

Marehemu Rudolph Chaula kushoto

Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe kimepata pigo kubwa kufuatia diwani wake wa kata ya Mlangali Rudolph Chaula maaarufu kwa jina la Kacheche kujinyonga .

Kadiri ya taarifa zilizotufikia na kuthibitishwa na katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eva Degeleki zinadai kuwa diwani huyo amekutwa akiwa kajinyonga katika moja kati ya vyumba vya nyumba yake ambavyo katika enzi ya uhai wake alikuwa akitumia kama ofisi yake ya udiwani.

Katibu huyo wa CCM Ludewa amesema kuwa hadi sasa hana taarifa za chanzo cha kifo chake ila anataarifa ya kujinyonga kwa diwani huyo na kuwa amepokea taarifa hiyo mida ya saa 8.15 usiku huu kujulishwa juu ya kifo hicho.


Imedaiwa kuwa diwani huyo toka mida ya mchana familia yake ilikuwa ikimsaka bila mafanikio baada ya wageni kufika kumuulizia na jitihada za kumtafuta huku na kule zilimezaa matunda usiku huu baada ya kuwa na wazo la kuvunja chumba hicho na kumkuta diwani huyo akiwa kajinyonga.

No comments:

Post a Comment