Friday, 30 August 2013

Tanzanian Blog Awards 2013. Nominate Us!!


Ndugu wasomaji wetu,
Timu ya sokonibongo.blogspot.com inayo heshima kubwa kuwashukuruni  sana kwa ushirikiano wenu kuendelea kufuatilia nini tunawaletea kila siku.
Tunasema asanteni sana nasi tunaahidi kuendelea kuwaleteeni taarifa hizi za kazi na nafasi za ufadhili wa masomo. Tunashukuru kwa wale wanaotuandikia kushukuru kwa mafanikio yao kupitia blog yetu, kama na wewe ni mmoja wao usisite kutuandikia ushuhuda wako, (testimonial) tutafurahi sana na kuwashirikisha wadau wetu.
Mwaka jana 2012 kupitia juhudi zenu mlituwezesha kunyakua tuzo ya Blog bora kabisa ya ujasiriamali nchini Tanzania (Best Entrepreneurial Blog 2012). Haya yalikuwa mafanikio mazuri blog yetu ikiwa na mwaka mmoja tu. Tuliwashukuru na tunaendelea kuwashukuru wasomaji wetu. Bofya hapa kwa habari zaidi kuhusu shindano la mwaka jana.
Sasa kipyenga kimepulizwa tayari kwa mtanange wa mwaka huu 2013. Nasi kama Sokonibongo Blog (Scholarship and Jobs in Tanzania) tunapenda kuwashirikisha wasomaji wetu katika mchakato huu wa kutupendekeza na hatimaye kutupigia kura kwa tuzo hizi.
Tanzanian Blog Awards (http://tanzanianblogawards.blogspot.com/) wamebadilidha kidogo utaratibu na vipengele, hivyo tungependa kuviweka wazi vipengele ambayo tungependa kugombania tuzo, navyo ni:-
  • Best Educational Blog
  • Best Business Blog
  • Best General Blog
Mwanzo wa kupokea mapendekezo hayo ni
Tarehe 17/8/ 2013 saa 12:01am mpaka tarehe 30/8/2013 saa 11:59pm saa za Africa mashariki.

Namna ya Kupendekeza (how to nominate)  
 nomination@bloggersassociationoftanzania.com au tanzanianblogawards@gmail.com
Unaweza kutuma email yenye Subject "www.sokonibongo.blogspot.com"  halafu kwenye body utacopy na kupaste au utaandika vipengele tunavyotaka kugombania ambavyo ni:-
  • Best Educational Blog
  • Best Business Blog
  • Best General Blog
 Kirahisi zaidi unaweza kucreate mail direct hapa au kama ni ngumu kwako basi usisite kuingia katika mail yako na kutupendekeza kwa utaratibu ulioelekezwa.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati

No comments:

Post a Comment