Tuesday 21 February 2012

YEMEN KUPATA RAIS LEO

Raia wa Yemen wanaamkia katika vituo vya kupigia kura kumchagua rais wao mpya, leo Jumanne.

Wafuasi wa Abd Mansour Hadi katika kampeni
Lakini kila mtu anajua kuwa atakayeshinda ni makamu wa Rais Abd Rabbu Mansour Hadi.
Yeye ni mgombea wa pekee. Hana mpinzani.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya mwaka mmoja wa ghasia na maandamano ya kupinga utawala wa Rais Ali Abdullah Saleh.
Kampeni zimekuwa zikiendelea kumuunga mkono makamu wa rais Abd Rabbu Mansour Hadi.
Mshindi wa tuzo ya Nobel raia wa Yemen Bi Tawwakol Karman amewataka raia wote wa Yemen kujitokeza kumuunga mkono Makamu huyo wa Rais, Bwana Hadi.
“Tunawaumba watu wote wa Yemeni wakiwemo vijana wajitokeze hii leo tarehe 21 Februari, sio kuunga mkono uchaguzi peke yake, bali kumuunga mkono Masour Hadi kuwa Rais wa mpito katika kipindi hiki cha mpito”
Huku Mshindi huyo wa Tuzo ya Nobel akimpigia debe Bwana Mansour Hadi ghasia zimeanza upya nchini Yemen.
Pia kumeripotiwa mfululizo wa milipuko na mashambulio katika vituo vya kupigia kura na sehemu nyingine.
BBC-SWAHILI

No comments:

Post a Comment