Saturday 22 September 2012

KILIMANJARO LAGER YAKABIDHI MABASI YA KIFAHARI KWA SIMBA NA YANGA

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager leo imetoa mabasi mawili kwa klabu za Simba na Yanga. Mabasi hayo ya kifahari yana thamani zaidi ya Sh milioni 450.

  Mabasi ya Simba na Yanga yakiwasili katika eneo la makabidhiano.PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Makao Makuu ya TBL, mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche pamoja na makundi ya Simba na Yanga pamoja, wadau mbalimbali wa mpira wakiwemo pia waandishi wa habari. Kununuliwa kwa mabasi hayo kumefanywa na TBL kwa mujibu wa mkataba baina yake na klabu hizo kubwa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu alisema: “Tunaona heshima kubwa sana kuwa na uhusiano na klabu hizi ambazo daima zina mafanikio.
“Malengo yetu ni kukuza soka nchini Tanzania na kwa kuanzia tumeona tushirikiane na Simba na Yanga ambazo kila zinapokutana uwanjani hali huwa ya kuchangamka sana katika mwendelezo wa Ligi Kuu.”
Alisema mabasi hayo yaliyotolewa kwa klabu hizo, yalenge kuinua soka na kuzitaka klabu hizo kuyatunza mabasi hayo kwa maslahi ya wachezaji na watendaji wengine. “Tutaendelea kuwapa msaada pale kwa vile tunatarajia kuwa mtaleta faida kwa maana ya matokeo mazuri katika soka kwa kutwaa mataji na kama wengi tujuavyo, mpira ni mabao.”
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema mabasi hayo yenye uwezo wa kubeba watu 51 yamenunuliwa kutoka Yutong.


Alisema mabasi hayo ni ya kisasa kabisa kwani yanabeba abiria 51 akiwemo dereva, ni imara kwani chasis yake ni 4x2, injini ya mabasi haya ni aina ya 300 HP Cummins, yana retarder ya umeme and breki aina ya ABS, yana TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika nane, milango na mabuti ya kisasa, kioo cha kuangalia nyuma kinachotumia umeme, jokofu na kiyoyozi.
“Tunataka wachezaji wetu wawe na raha wanaposafiri. Hii ndiyo maana tumeamua kutoa mabasi haya ya kifahari ambayo ndani yake kuna huduma muhimu kama televisheni, friji, vitu ambavyo tunaamini mtavitunza.”
Aliongeza kuwa pamoja na ukweli kwamba TBL inawajibika kununua mabasi hayo kwa mujibu wa mkataba, lakini lengo kuu ni kuona kuwa wachezaji wanakuwa katika mazingira mazuri.
Baada ya makabidhiano hayo, wahudhuriaji kutoka klabu hizo walicheza na kufurahia mabasi hayo huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Bia ya Kilimanjaro ilianza kuzidhamini Simba na Yanga tangu mwaka 2008.
Kuhusu TBL
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni watengenezaji na wauzaji wa bia safi pamoja na vinywaji mbalimbali visivyo na kileo. TBL ina hisa katika Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited na Kampuni Mama ya Mountainside Farms Limited.
Baadhi ya vinywaji ni pamoja na Balimi Extra, Eagle, Eagle dark, Bia Bingwa, Maji ya Safari, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Kilimanjaror, Castle, Castle Milk Stout, Redd’s Original, Grand malt, Miller Ginuine Draft, Peroni. Vingine ni Konyagi Gin na Amarula Cream.
TBL imo katika orodha ya Soko la Hisa la Dar es Salaam huku ikiwa na wafanyakazi wapatao 1,300. Ina mawakala na wasambazaji kote nchini na viwanda vitatu makini.

No comments:

Post a Comment