Saturday, 22 September 2012

Julius Malema matatani kwa utata wake~BBC

Polisi wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa mwanasiasa wa Afrika kusini anayeleta utatanishi, Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Bwana Malema.
Bwana Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa kupinduliwa.

No comments:

Post a Comment