Wednesday, 4 July 2012

Shukrani kwa waliowezesha blog letu kunyakua tuzo....!!!!!


Wiki mbili zilizopita tuliandika kuomba kura zenu wasomaji wetu, tulikuwa tukigombania tuzo ya blog bora Tanzania shindano linalosimamiwa na Tanzania Blog Awards chini ya udhamini wa Kinawaka Inc. Mchakato ulikuwa mrefu tangu uteuzi hadi kupiga kura na hatimaye kutawazwa washindi wa tuzo hizo.
Tulitajwa katika kipengele kimoja tu ambacho ni "Best Entrepreneurial Blog" ushindani ulikuwa mkali ukihusisha blog 5 yetu ikiwa mojawapo. Mwisho wa kura blog yetu ilichukua 63.18% ya kura zote katika hicho kipengele. Natumia fursa hii kuwashukuruni nyote kwa mchango wenu hadi kutufikisha katika mafanikio haya. huu ni mwanzo tu tunawaahidi kuwaletea kile mnachokitafuta. Tunathamini sana michango na mawazo yenu tunafanyia kazi kila maoni mnayoyaleta hivo basi jisikieni huru kuuliza au kutoa maoni katika lolote mtakaloliona kwa sababu tuna taarifa muhimu kuzihusu.
Kwa matokeo zaidi ya shindano bofya hapa
Asanteni sana kutuweka


No comments:

Post a Comment