Tuesday, 8 May 2012

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LULU, SASA AMGEUKIA MUNGU!!

Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo

Katika hali ya kustaajabisha!!
IMEBAINIKA kuwa wasanii wawili maarufu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Kajala Masanja ambao sasa wako katika matatizo wakikabiliwa na tuhuma mbili tofauti sasa wamemgeukia Mungu.
Inasemekana kuwa mara baada ya kukutana gerezani na kuombewa na waumini wa Kanisa la Efatha wamekuwa wakishinda wakisoma Biblia.
Habari zinasema licha ya kusoma kitabu hicho kitakatifu kwa waumini wa Kikristo, wasanii hao wamekuwa wakivaa rozali wakati wote badala ya cheni za dhahabu ambazo walikuwa wakivaa walipokuwa uraiani.
“Hivi sasa wamekuwa wakining’iniza rozali shingoni badala ya kuvaa mikufu ya dhahabu, na wamekuwa wakisoma sana Biblia wakiamini kuwa Mungu atawasaidia katika matatizo yao, hakika nakuhakikishia kuwa sasa wamebadilika sana,” kilisema chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment