Friday 9 March 2012

MAHAKAMA KUU YASITISHA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI

Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Jana (Alhamisi Machi 8, 2012) ilitoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu (Jumatano Machi 7, 2012).
Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.
Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.
SOMA ZAIDI